MAHAKAMA YAMUACHIA HURU DIANE NA MAMA YAKE

Diane Rwigara baada ya kuachiliwa

Mahakama mjini Kigali, Rwanda imetangaza kwamba mwanasiasa Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara hawana hatia na kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.

Mahakama imesema kwamba imefanya uamuzi huo kutokana na kwamba upande wa mashitaka haukutoa ushahidi wa kutosha.Diane Rwigara

Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Muendesha mashtaka alikuwa ameomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela.

Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa. Marekani imeishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo, lakini Rwanda imejibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe.Mama yake Diane, Adeline Rwigara

Uamuzi huo ulikuwa wa mwisho kuhusu maombi ya upande wa mashitaka ya kuwapa kifungo cha miaka 22 jela katika kikao cha mwisho mwezi uliopita, huku upande wa mawakili wao wakipinga maombi hayo na kusisitiza wateja wao kuachiwa huru mara moja.Image captionSherehe mahakamani baada ya wawili hao kuachiliwa

Waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini.

Kadhalika Diane Rwigara na Mamake walishitakiwa kuchochea chuki na kusambaza uvumi kwa lengo la kuhamasisha umma kugoma dhidi ya utawala.

Uamuzi wa leo ulisubiriwa kwa hamu na gamu baada ya Diane Rwigara na mamake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hii wakiwa hawako kizuizini.Diane Rwigara akisherehekea

Kwa mshangao wa wengi , mapema mwezi wa 10 mwaka huu mahakama ilichukua uamuzi wa kuwaachilia huru kwa dhamana ikisema sababu za kimsingi zilizosababisha kesi yao kusikilizwa wakiwa kizuizini hazipo tena.

Wao Wanakanusha mashtaka dhidi yao wakisema yalichochewa kisiasa hasa baada ya Diane Rwigara kujitokeza katika ulingo wa kisiasa,akipinga wazi sera za chama tawala na kutaka kugombea urais katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527