BEN POL AKUTANA NA MEMPHIS DEPAY


Ben Pol akiwa na Memphis Depay

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amekutana uso kwa uso na mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye hivi sasa anachezea klabu ya Olympique Lyon, Memphis Depay.

Ben Pol ambaye yupo Dubai, amekutana na mchezaji huyo katika moja ya maeneo tulivu ya mji huo na kuiweka picha yao wakiwa pamoja katika mtandao wa Instagram.

Katika picha hiyo, Ben Pol ameambatanisha maneno yanayosema, "nimekutana na Memphis Depay tukiwa tunaelekea kupata chakula cha mchana".

Memphis Depay alichezea klabu ya PSV Eindhoven kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2015 ambako alicheza mechi 33 na kufunga mabao 2. Mwaka 2017 alijiunga na Lyon ya nchini Ufaransa, ambapo mpaka sasa amecheza mechi 69 na kufunga mabao 29.

Ben Pol amekuwa katika ziara mbalimbali barani Ulaya na Asia tangu mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo pamoja na mambo mengine, amekuwa akifanya matamasha mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527