ALIKIBA ATOA OFA KWA DADA ALIYEMLILIA

Msanii Alikiba ameamua kutoa ofa kwa dada Emiliana Mgema aliyemlilia juzi kwenye tamasha la Tigo Fiesta


Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ali Kiba ametangaza ofa hiyo huku akiwa ameweka video ya dada huyo akiwa anahojiwa huku analia na kueleza hisia zake jinsi anavyompenda msanii huyo.

Ali Kiba ameandika “Asante sana dada anayemjua huyu dada amwambie nina tiketi yake ya bure na mofaya zake za kutosha tarehe 29 /12 Next Door Arena,” aliandika Kiba wakati anatangaza ofa hiyo kwa Emilina ambapo anatarajia kufanya shoo yake aliyoipa jina la ‘Funga mwaka na KingKiba.’

Emy amesema ameanza kumpenda Ali Kiba tangu alipotoa kibao chake cha Macmuga ambapo kipindi hicho alikuwa akisoma darasa la saba Shule ya Msingi Nata mkoani Tabora na kuanzia hapo amekuwa akimfuatilia hadi leo na hakuna ngoma yake hata moja aliyowahi kuiona mbaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post