SIMBA YASHUSHA BEKI MATATA KUTOKA BURKINA FASO KUMRITHI KAPOMBE


Mchezaji Zana Coulibaly raia wa Burkina Faso anatarajia kutua leo nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili na Simba akitokea timu ya ASEC Mimosas kwa ajiri ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho. 

Coulibaly ambaye anakuja kuziba nafasi ya Shomari Kapombe ambaye amepata maumivu ya mguu alipokuwa kwenye kambi ya timu ya taifa nchini Afrika Kusini, hivyo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Simba kupitia kwenye ukurasa wa kwenye mtandao wao wa kijamii wa Instagram wamethibitisha ujio wa mchezaji huyu ndani ya kikosi cha kama sehemu ya kukifanyia maboresho kuelekea michezo ya ligi kuu bara na ile ya klabu bingwa Afrika.

“Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo atawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za mwisho kujiunga na timu yetu ili kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha.”

Simba huu ndiyo utakuwa usajili wao wa kwanza toka kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajiri 15, Novemba, 2018, huku leo wakitarajia kucheza mcherzo wao wa hatua ya awali ya michuano ya kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mbambane Swallows kutoka Swaziland kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527