WATU 30 WAFARIKI ZIWA VICTORIA


Zaidi ya watu 29 wamethibitishwa kufa maji katika ziwa Victoria baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama huko nchini Uganda.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili ya Novemba 25, 2018, huku mashua hiyo ikiwa kwenye safari ya kutoka Port Bell Luzira kuelekea kisiwa cha Mutima.

Maafisa wa usalama wa nchini Uganda wamesema kwamba chanzo cha mashua hiyo kuzama ni uzito uliopitiliza, na mpaka sasa watu 29 wameshaokolewa.

Taarifa zaidi zinasema kwamba mashua hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya 100, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya vifo ikaongezeka.

Ajali za maji zinazosababisha vifo katika ziwa Victoria zimekuwa zikitokea mara kwa mara, ambapo hivi karibu Tanzania ilipoteza zaidi ya watu 200 kutokana na kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe.
Miongoni mwa watu waliofariki kwenye ajali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527