WACHINA WATUPWA JELA MIAKA MIWILI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka miwili jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3 wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol (T) Investment Ltd baada ya kukiri makosa ya kushindwa kuchukua tathmini ya uaribifu wa mazingira.


Washtakiwa hao ni Injinia Xia Yanan (26), Chen Jinchuan (31) na Mtala Habibu (29) fundi umeme.Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga kuwasomea washtakiwa makosa yao na kukiri.


Hakimu Shaidi amesema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao anawahukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni Tisa na Laki Tatu ama kwenda jela miaka 2 kwa washtakiwa wote.


Washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka wanadaiwa kati ya January na August 28,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni ambapo waliendeleza ujenzi bila kuchukua tahadhari ya mazingira kutoka NEMC.


Pia wanadaiwa kutenda kosa la kutotii amri (NEMC) August 25,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walishindwa kutii amri halali kupitia barua ya NEMC ya kusimamisha ujenzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527