DC MAGEMBE AYATAKA MASHIRIKA YANAYOJIHUSISHA NA UKIMWI KWENDA UKEREWE



Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza,Cornel Magembe ameyataka mashirika na taasisi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuelekeza nguvu zaidi wilayani humo ili kutokomeza maambukizi ya VVU. 

Magembe ametoa ombi hilo leo Jumanne Novemba 6,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza kinachoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella. 

Alisema mashirika mengi yamekuwa yakielekeza nguvu maeneo ya mjini na kusahau maeneo ya pembezoni wakati watu waishio vijijini huingia mjini na kusababisha maambuzi kuendelea kuwepo. 

“Tunaomba wadau mje Ukerewe kwani wananchi wanahitaji kupewa elimu kuhusu VVU na UKIMWI,huku pia kuna maambukizi,huku wengine wakiona mtu ni mnene wanaamini hana maambukizi,hivyo maambukizi ya VVU yanaendelea kuwepo”,alieleza

“Watu wa Mjini wana uelewa kuhusu VVU na UKIMWI lakini Vijijini bado hawajawa na elimu,hivyo ni vyema wadau yakiwemo mashirika yakaelekeza nguvu pia kwenye maeneo ya pembezoni ili tuweze kutokomeza maambukizi ya VVU Mjini na Vijijini”,aliongeza Magembe. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza,Cornel Magembe akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza leo - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527