Friday, November 30, 2018

MHADHIRI ALIYESEMA UDSM IMEKITHIRI KWA RUSHWA YA NGONO AITWA KUHOJIWA

  Malunde       Friday, November 30, 2018
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Vicensia Shule ameitwa kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho kuhojiwa leo Ijumaa, Novemba 30, 2018 mchana kuhusiana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mtandao wa Twitter akimuomba Rais Dkt. John Magufuli kuingilia kati kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Vicensia aliandika; "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli." 
Jana Alhamisi jioni aliandika kwenye Twitter kwamba amepigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili UDSM.

"“My good people, a quick update. Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi. For our dear sexual violence survivors, we are almost there, we will win, big time! #IStandWithDrShule,” Aliandika
Ingawa hakueleza ni rushwa ya aina gani iliyokithiri, lakini katika baadhi ya vyuo vikuu vingi kumekuwepo na tatizo la wahadhiri kuwarubuni wanafunzi kwa rushwa ya ngono ili wawafaulishe na pindi wanapogoma hupigwa sup, carryover.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post