MKAPA KUAGWA RASMI UDOM KESHO

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambaye pia ni Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa kuagwa rasmi kesho chuoni hapo baada ya kumaliza kipindi chake.

Rais Mkapa amekuwa mkuu wa chuo hicho tangu kianze mwaka 2007 hadi sasa.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Peter Msoffe, akizungumza na waandishi wa habari, alisema ataagwa kwenye mahafali ya tisa yanayotarajiwa kufanyika Novemba kesho chuoni hapo.


Alisema kwa mujibu wa hati idhini ya chuo, Mkapa anatarajiwa kumaliza muda wake Machi 2019 na kwamba kwa kuwa ni mahafali yake ya mwisho, wameamua kumuaga kesho.


Alisema Mkapa ameshakitumikia chuo kwa kipindi cha miaka 11 zikiwa ni awamu mbili tangu kuanzishwa kwake.


Alisema UDOM itaendelea kuvuna busara zake hata baada ya kumaliza na amekuwa nguzo imara ya chuo hicho.


Aidha, Prof. Msoffe alisema katika mahafali hiyo ya tisa ya mwaka huu kutakuwa na jumla ya wahitimu 7,122 kwa ngazi mbalimbali.


Alisema mahafali hiyo itatanguliwa na kongamano la tisa la chuo hicho litakalofanyika leo na litakaloongozwa na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ambaye atawasilisha mada juu ya maisha ya mwanzilishi wa Taifa la India, Mahatma Gandhi na mchango wake katika jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527