MKUU WA MKOA WA TABORA AWATAKA WAENDESHA BODABODA KUNUNUA PAFYUMU WATEJA WASHANGAE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 21, 2018

MKUU WA MKOA WA TABORA AWATAKA WAENDESHA BODABODA KUNUNUA PAFYUMU WATEJA WASHANGAE

  Malunde       Wednesday, November 21, 2018

Mkoa wa Tabora umejipanga kutoa huduma za uhakika pamoja na usalama katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo Jumatano wakati wa jukwaa la fursa za uwekezaji na biashara linalotarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza mjini Tabora Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri amewahakikishia wageni zaidi ya 500 watakaohudhuria watakuwa salama na kupewa huduma iliyo bora, na kusema tayari wamezungumza na watoa huduma ya usafiri wa bodaboda kuwa waaminifu kwa wateja wao pale watakaposahau mali zao.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

"Kwa wale watakaosahau mkoba kwenye bodaboda watajikuta wanapelekewa mikoba yao na waendesha bodaboda kwani hivyo ndivyo tulivyojipanga, pia nimezungumza na waendesha bodaboda kununua pafyumu kila mtu ili wateja wao washangae na kutoisahau Tabora" amesema Mwanri.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka wananchi na wajasiriamali kuitumia fursa hiyo kikamilifu kujiongezea kipato ili kupambana na umaskini.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post