KESI YA UCHOCHEZI BADO INAWANYEMELEA MBOWE NA WENZAKE MAHAKAMA YAAGIZA KUKAMATWA



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hati ya kukamatwa kwa Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, kujieleza kwanini wasifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika kusikiliza kesi yao. 

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Matiku pamoja na viongozi wengine wa Chadema wanakabiliwa na kesi ya uchochezi.

Amri hiyo ilitokana na jopo la Mawakili wa Jamhuri likiongozwa na Mawakili wa Serikali Wakuu, Faraja Nchimbi, Dk. Zainabu Mango na Wakili wa Serikali Jackline Nyantori, kuomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa washtakiwa hao.

Maombi hayo yaliwasilishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Hakimu alisema taarifa za mdhamini wa mshtakiwa Mbowe zinajichanganya na kudai kuwa Novemba Mosi, mwaka huu, mdhamini alidai mahakamani kuwa mshtakiwa yuko mahututi amepelekwa kwenye matibabu Afrika Kusini na mahakama ilimwamini na akaahidi kupeleka vielelezo.

"Mahakama ilimwamini mdhamini kwamba ataleta vielelezo vya matibabu ya Mbowe, lakini leo (jana), anasema amekwenda kutibiwa Dubai, inaonyesha wazi mdhamini si mwaminifu, mshtakiwa Matiko anakosa kuhudhuria kesi yake mara kwa mara na amesafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama, anatumia vibaya haki yake ya kikatiba ya dhamana," alisema hakimu wakati akitoa amri dhidi ya washtakiwa hao.

Alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Novemba 22, mwaka huu.
Via:Nipashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post