WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AFYEKELEA MBALI SWALI LA MTEGO LA ZITTO KABWE


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameshindwa kujibu kipengele B kwenye swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuhusiana na idadi ya mashauri yaliyofunguliwa katika mahakama za kimataifa, ambayo serikali imeshinda na kushindwa.


Zitto leo tarehe 9 Novemba 2018 amehoji bungeni kuwa, “Je kuanzia mwaka 2000 hadi 2018 kumekuwa na mashauri mangapi dhidi ya Jamhuri ya Muungano, mangapi yameamuriwa, mangapi bado na mangapi Tanzania ilishinda.”

Lakini Prof. Kabudi hakujibu swali hilo, akisema kwamba ni la mtego na hivyo hatauingia kamwe mtego huo.

Prof. Kabudi ameeleza kuwa, serikali haita tamka chochote kuhusu kesi zilizofunguliwa kwenye mahakama za kimataifa, kwa kuwa ikitoa tamko na kuingia katika taarifa za bunge (Hansard) litahatarisha hoja za serikali katika kesi hizo.

“Masuala yote aliyoyasema, yale yaliyo katika mahakama za kimataifa serikali haitamka chochote. Nataka niwambie katika sheria za kimataifa tamko lolote nitakalolifanya hapa likaingia kwenye hansard litahatarisha hoja za serikali kwenye kesi hizo, na mtego huo uwe wa bahati mbaya au wa kutumwa sitaungia kamwe,” amesema Prof. Kabudi.
Chanzo - Mwanahalisi online

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527