Wednesday, November 28, 2018

SIMBA SC WAICHAPA MBABANE SWALLOWS 4-1

  Malunde       Wednesday, November 28, 2018

Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuanza vizuri leo katika mchezo wa Fainali za Mabingwa ya Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows FC ya Swaziland.

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane.

Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1.

Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.

Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza.
Chanzo - Saleh Jembe blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post