SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za mfuko huo leo jijini Dodoma kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza na Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF Mkoa wa Dodoma leo alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

Na Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Jijini Dodoma,wametakiwa kutilia mkazo ulipaji wa mafao ya wastaafu kwa wakati.

Akitoa maagizo hayo leo jijini hapa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

Mhe.Mavunde amesema kuwa inatakiwa mlipe kwa wakati mafao kama ilivyo kauli mbiu yenu ya “Tunalipa Kuanzia jana” ili lengo la serikali la kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, litimie .

''Inatakiwa wastaafu wapewe umuhimu wa elimu kabla ya kuwalipa mafao ili waweze kujiandaa vyema kwa kuanzisha miradi na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha''amesema Mavunde

Aidha Mhe.Mavunde amewaagiza wafanyakazi wote kuhakikisha wanatoa huduma stahiki zenye ubora na kwa wakati ili kuisaidia serikali kusonga mbele katika huduma ya hifadhi ya jamii.

“Matarajio ni kwamba mtatoa huduma kwa ufanisi na kwa ubora ili yale matarajio ya serikali yaweze kutimia, awali kulikuwa na malalamiko watu hawapati huduma stahiki lakini naimani hakutakuwa na malalamiko hayo,”amesema Mavunde

Kwa Upande wake, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, amesema kuwa ofisi hiyo imeanza kufanya kazi zake Septemba mosi mwaka huu na kuna wanachama wanaochangia ni zaidi ya laki moja.

“Tumejipanga kuwahudumia ipasavyo na hadi sasa tumekusanya Sh.Milioni 880 katika mkoa wa Dodoma na tutaendelea kusimamia na kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria,”amesema Bandawe

Hata hivyo amebainisha kuwa hadi sasa wanachama 2792 wameshapita kupata huduma na wamepokea madai 796 ya wanachama wa mifuko mbalimbali iliyounganishwa kwenye mfuko huo.

Bandawe amesema kuwa madai 717 yameshughulikiwa na wanachama wamelipwa mafao yao na mengine 79 yapo kwenye hatua mbalimbali za kufanyiwa kazi katika mkoa wa Dodoma tu.

Aidha amesema takribani wastaafu 1027 wanatarajiwa kustaafu katika kipindi cha 2018/19 ambapo mfuko huo umejipanga kutoa elimu ya kujipanga na ustaafu wao ikiwemo kubuni miradi ya kujiimarisha kiuchumi kwa mkoa wa Dodoma peke yake

Bandawe amesema kuwa mkoa huo una wanachama Waajiri zaidi ya 227 na wanachama zaidi ya 100,000 unahudumia Wilaya saba, aidha amezungumzia kuhusu maendeleo ya jengo lao la kitega uchumi zilipo Ofisi za Mkoa PSSSF Plaza lenye ghorofa 11 kwamba limejaa kwa asilimia 100 na maendeleo ni mazuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post