WAFUGAJI WA NYUKI IRINGA KUNUFAIKA NA KAMPUNI YA RUAHA FARM


KAMPUNI ya uchakataji wa asili ya Ruaha farm mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha Honey imeanza kuwaokoa kiuchumi wafugaji wa nyuki mkoani Iringa kwa kutoa mizinga na kuwaunganisha na soko la asali. 

Kampuni ya Ruaha Farm imekuja kivingine baada ya kufunga mashine za kisasa za kuchakata asali yenye ubora pasipo kutumia vifaa vya kienyeji kama moshi na vingine.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ruaha Honey Fuad Abri alisema kuwa kampuni yake imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya Tanzania ya viwanda.

Alisema ubora wa asali ya kampuni ya Ruaha Honey ni tofauti na asali nyingine zinazouzwa mitaani kwani sifa kubwa ya asali ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park.

Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi wa uchakatishaji pamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia salama na rafiki kwa nyuki.

Alisema Ruaha honey ni asali ya kampuni ya ruaha farm pamoja na wafugaji wa nyuki wa vijiji vinavozunguka hifadhi ya ruaha. 

Kampuni ya Ruaha honey inashirikiana na wafuga nyuki wa Iringa kwa kuwawezesha kupata mizinga ya kisasa na kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ya ufugaji sahihi wa nyuki ili kulinda ubora wa mazao ya nyuki yanayopatikana kama asali na nta.

Ruaha honey pia inawapatia soko la asali wafugaji wa nyuki kwa lengo la kuinua kiuchumi kaya maskini kupitia ufugaji wa nyuki alisema Abri

Kuwa asali ya Ruaha ni asali halisi inayotokana na uoto asili wa miti ya Acacia, mibuyu na miti pori na maua pori hivyo ni asali bora zaidi .

Alisema kupitia kampuni ya Ruaha farm inafugia nyuki katika shamba lake liliopo Tungamalenga ambayo ni hifadhi ya nyuki ya kwanza binafsi Tanzania na Afrika mashariki

Lengo ni kuinua ufugaji wa nyuki wa nyanda za juu kusini pia kuendeleza ufugaji wa nyuki kisasa kama sehemu ya kuwa na viwanda bora vya mazao yatokanayo na nyuki.

Hifadhi ya nyuki ya Ruaha ni eneo linafanyika utafiti mbali mbali wa nyuki pamoja na mazao yake, pia ni shamba darasa kwa wafuga nyuki wengine wanaozunguka eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527