Picha : SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA

Shirika la Save The Children limekutana na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kuwaeleza hali halisi ya ndoa na mimba za utotoni zinazochangiwa na mila na desturi kandamizi katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Novemba 19,2018 katika ukumbi wa Good Shepherd mjini Kahama, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.

Akifungua mafunzo,Macha aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

Alisema katika wilaya ya Kahama,halmashauri za Msalala na Ushetu zinaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi kandamizi,umaskini,tamaa za mwili,mazingira pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo simu za mkononi zimekuwa zikiongeza tamaa kwa wanafunzi.

“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika vita hii ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa mnawafikia watu wengi zaidi kupitia habari zenu,Lazima wadau wote tushirikiane kutokomeza changamoto hizi ili watoto wetu wawe salama”,alisema.

Aidha Macha aliwataka wananchi kuzingatia utawala wa sheria na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia sheria watu wote wanaoshiriki kuwafanyia ukatili watoto.

Kwa upande wake,Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema lengo la kukutana na waandishi wa habari ni kufahamiana na kuwaeleza kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika ili kufanya kazi pamoja kuhakikisha mimba na ndoa za utotoni zinatokomezwa mkoani Shinyanga.

“Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,Save The Children imeona ni vyema kukutana na waandishi wa habari kwani tunaamini waandishi wa habari ni chachu ya mabadiliko katika jamii,hivyo tukiwaeleza hali halisi ya mimba na ndoa za utotoni mtaweza kuchukua hatua pia”,alieleza Malima.

Alisema shirika hilo linatekeleza miradi mitatu mkoani Shinyanga ambayo ni mradi wa elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.

“Tunashirikiana na shirika la AGAPE kutekeleza mradi wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwenye kata 12 na shirika la KIWOHEDE kwenye kata 8 katika halmashauri ya Ushetu ambapo katika maeneo kiwango cha mimba na ndoa za utotoni ni kikubwa”,alisema Malima.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children kwa ajili ya kukutana na kupanga mikakati ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima - Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu- Malunde1 blog.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la shirika hilo kutoa mafunzo kwa waandishi yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la mafunzo hayo.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akielezea miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari Malaki Philipo na Stephen Wang'anyi (kulia) wakiwa ukumbini.
Mratibu wa mradi wa Ulinzi wa mtoto wa shirika la Save The Children,Alex Enock akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mafunzo yanaendelea....Kulia ni Salim Yasin kutoka Huheso Fm akifuatiwa na Simeo Makoba wa Radio Faraja Fm na Marco Maduhu wa gazeti la Nipashe.
Kushoto ni Mwandishi wa habari Paulina Juma kutoka Kahama Fm na Kadama Malunde wa Malunde1 blog wakiwa ukumbini.
Kushoto ni Afisa mradi wa kuzuia mila na desturi kandamizi kutoka shirika la Save The Children,Msemakweli Bitagatcha na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi,Shija Felician na Shaban Alley wa Star Tv wakifuatilia mada ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Kushoto ni Mdhibiti Ubora wa miradi kutoka Save The Children Kanuty Munishi akifuatiwa Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la KIWOHEDE,Victor Reveta na Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE ,Peter Amani wakiwa ukumbini. 
Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron na Mtathmini na Ufuatiliaji wa miradi wa shirika la KIWOHEDE, Beatrice Freedom.
Kushoto ni Mwandishi wa habari/Mkurugenzi wa Kijukuu blog,William Bundala akifuatiwa Greyson Kakuru wa TBC.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akitoa mada kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Kulia ni Afisa Habari halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Emmanuel Shomary akifuatiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Ushetu,Jovitus George wakifuatilia mada ukumbini.
Kulia ni mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Frank Mshana na Sumai Salum kutoka Divine Fm wakifuatilia mada ukumbini.
Maafisa kutoka shirika la Save The Children,KIWOHEDE na AGAPE wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la KIWOHEDE,Victor Reveta akielezea mafanikio ya mradi huo katika halmashauri ya Ushetu.
Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la AGAPE ,Peter Amani akielezea mafanikio ya mradi huo katika halmashauri ya Kishapu.
Kushoto ni Afisa Habari halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Robert Hokororo akiwa ukumbini,wengine ni waandishi wa habari.

Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527