NAIBU WAZIRI WA UJENZI APATA AJALI SINGIDA

Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye jana Jumapili Novemba 11, amenusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.

Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.

“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527