MUGABE NI MGONJWA...HAWEZI KUTEMBEA

Mugabe alienda kupiga kura mwezi Julai akiwa na mke wake Grace (kushoto)


Rais wa zamani wa Zimbawe Robert Mugabe, 94 hawezi kutembea kutokana na afya yake ilidhoofika, kwa mujibu wa Rais Emmerson Mnangagwa.

Bw Mugabe amekuwa nchini Singapore akipata matibabu kwa ugonjwa usiojulikana katika kipindi cha miezi miwili liyopita.

Rais huyo wa zamani pia alifanya safari kadhaa kwenda kupata matibabu wakati wa siku za mwisho za uongozi wake.

Bw Mnangagwa alichukua usukani kama rais mwaka mmoja uliopita baada ya Bw Mugabe kuondolewa madarakani jeshi lilipoingilia kati.

Hadi kipindi hicho Mugabe alikuwa amekaa madarakani kwa miaka 37 kwanza kama waziri mkuu na kisha kama rais.Rais Emmerson Mnangagwa

Rais Mnangagwa alikuwa akiongoza mkutano sehemu moja iliyo nyumbani kwa Mugane wakati alizunguzia afya ya mtangulizi wake.

"Sasa yeye ni mzee, na hawezi kutembea lakini chochote anachokitaka tunampa," AFP ilimnukuu akisema.

Wakati Mugabe alikuwa madarakani maafisa walisema alikuwa akitibiwa matatizo ya macho na kukana madai kuwa alikuw akiugua saratani.

Licha ya kushindwa kutembea, Bw Mnangagwa alisema kiongozi huyo wa zamani anahisi vizuri na atarudi nyumbani wiki ijayo.

"Tunamhudumia. Ni yeye mwanzilishi wa taifa la Zimbabwe, Yeye ni baba yetu wa Zimbabwe iliyo huru," Rais aliongeza.

Serikali inagharamia matibabu ya Mugabe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527