MKE WA MWALIMU WA CHUO CHA VETA AJIUA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, November 15, 2018

MKE WA MWALIMU WA CHUO CHA VETA AJIUA

  Malunde       Thursday, November 15, 2018
Mke wa mwalimu wa Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Manyara, Judith Uromi (32) amekufa kwa kujinyonga na kanga aliyofunga dirishani chumbani kwake kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa ndoa.Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga alisema kilitokea Novemba 10, mwaka huu, saa 1:30 jioni katika maeneo ya Wang’waray karibu na chuo cha Veta wilayani Babati.

Alifafanua kuwa Uromi aliwaaga wanafamilia anaingia chumbani kupumzika saa 12:00 jioni wakati huo mumewe akiwa ametoka na mgeni kwa lengo la kumsindikiza. Hakutoka ndani mpaka alipogundulika amekufa.

Kwa mujibu wake, chanzo cha uamuzi huo wa kujinyonga haujulikani kwani hakuacha ujumbe wowote. Pia alisema Uromi ameacha watoto wawili wa kiume na mwili wake haukuwa na majeraha yoyote.

Chanzo : Habari leo
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post