Wednesday, November 28, 2018

MGOMO WA MAGARI YA ABIRIA WASITISHWA BUKOBA

  Malunde       Wednesday, November 28, 2018
Mgomo wa madereva wa magari ya abiria uliodumu kwa masaa kadhaa na kusababisha abiria kushindwa kusafiri kutoka manispaa ya Bukoba kwenda wilaya mbalimbali za mkoa wa Kagera umemalizika baada  serikali ya wilaya na viongozi wa madereva kukaa meza moja ya mazungumzo na kufikia muafaka.


Jana madereva wa magari hayo walifanya mgomo wa kutoa magari yao katika kituo cha mabasi cha manispaa ya Bukoba wakipinga hatua ya kupandishiwa ushuru bila wao kushirikishwa.

Katibu tawala wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala amesema katika kikao walichokaa na viongozi wa madereva na wadau wengine wa usafiri wamekubaliana masuala kadhaa ambayo madereva hao wanahitaji yafanyiwe kazi ikiwamo kituo hicho kuwekewa lami.

“Wanasema pia magari madogo yanayobeba abiria yaondolewe maana hayalipi kodi, vijengwe vyoo na miundombinu nyingine,  kwa hiyo tumekubaliana waendelee na viwango vya  zamani vya shilingi 1,000 kwa Hiace na shilingi 2,000 kwa Coaster, halafu tukutane tena Desemba 6 mwaka huu, ndipo tutaelezana  masuala yapi yatatekelezwa na yapi hayatatekelezwa”, amesema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post