MBOWE ATUPWA GEREZANI...ASEMA 'KESHO NI NZURI KULIKO JANA...MSIOGOPE'

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kuwa “imara na kutoogopa” akisema kesho ni “nzuri kuliko jana” baada ya kufutiwa dhamana yake.

Mbowe ametoa kauli hiyo, akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, baada ya mahakama hiyo kumfutia dhamana na mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana hiyo.

Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alitumia kizimba cha mahakama hiyo kusalimiana na viongozi wengine wa Chadema na wafuasi pamoja na kutoa ujumbe wake wa kuwatia moyo.

“Naomba muwe stable (imara), msiogope. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Mbowe kisha akamalizia na salamu ya chama hicho ya “peoples” na wafuasi kuitikia “power”.

Kabla ya kutoa ujumbe huo, askari walitaka kumuondoa katika kizimba, lakini akawasihi akisema “kwanza nizungumze na watu wangu”.

Uamuzi wa kuwafutia wawili hao dhamana ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri akisema kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao ni kudharau amri za mahakama kwa makusudi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527