ZIFAHAMU BAADHI YA REKODI ZA WAPINZANI WA SIMBA MBABANE SWALLOWS

Wawakilishi wa kwanza wa Tanzania katika michuano ya vilabu barani Afrika, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi mnono nyumbani wa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli hapo jana, ambapo leo ni zamu ya wawakilishi wa pili Simba itakapovaana na Mbabane Swallows ya Swartzland.
Kuelekea mchezo huo, hizi hapa ni baadhi ya rekodi za wapinzani hao wa Simba pamoja na ubora wao katika misimu kadhaa ya karibuni.

Mbabane Swallows ni timu iliyojipambanua vizuri katika ligi kuu nchini Swartzland, ambapo imefanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi katika miaka miwili mfululizo bila kupoteza mchezo wowote.

Msimu wa 2016/17, Mbabane Swallows ilishinda ubingwa kwa alama 60, huku ikimpita mshindani wake wa pili kwa tofauti ya alama 23. Katika msimu wa 2017/18 pia ilishinda ubingwa kwa jumla ya alama 60 huku mshindani wake wa pili akiachwa kwa tofauti ya alama 8.

Msimu uliopita, iliishia katika hatua ya makundi ya michuano ya shirikisho barani Afrika, timu ambazo zilifuzu hatua ya 16 bora katika kundi lake ni CS Sfaxier na MC Alger huku yenyewe pamoja na Platinum Stars ya Afrika Kusini zikiondoshwa katika mashindano.

Kikosi chake kina wachezaji watatu wa kigeni ambao ni, Umukoro Stanley wa Nigeria, Amuogou Jean wa Cameroon na Tarawallie Sallieu wa Sierra Leone.

Kwa haraka haraka timu hii inaonekana kuwa ni ngumu kuifunga au kuruhusu mabao inapokuwa katika uwanja wa nyumbani, Jambo ambalo kocha wa Simba, Patrick Aussems anapaswa kuliangalia kwa jicho la tatu bila kujali ubora ua udhaifu wa ligi yao.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527