MAMBO BADO MAGUMU KWA MBOWE.....SERIKALI YAWASILISHA KUSUDIO LA KUKATA RUFAA

Hukumu juu ya maamuzi ya kupewa au kutopewa dhamana kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko imeonekana kuwa ngumu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu.

Jamhuri imetangaza nia hiyo baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, kutupilia mbali baadhi ya hoja zao kwa kile alichokieleza kukosa msingi wa kisheria.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya kutosikilizwa kwa rufaa hiyo dhidi ya washtakiwa Mbowe na Matiko kwa kile walichokisema kuwa baadhi ya vipengele vya kisheria ambavyo vilitumika vinainyima sifa mahakama hiyo kusikiliza rufaa.

Kwa upande wa mawakili wa watuhumiwa Mbowe na Matiko walieleza kupinga taarifa hiyo ya rufaa kwa kile walichokidai kuwa upande wa jamhuri haujafuata baadhi ya taratibu za mahakama.

Mbowe na Matiko ni miongoni mwa viongozi saba, ambao wanakabiliwa na kesi ya msingi ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi Chuo Cha Usafirishaji cha NIT, Akwilina Akwilini pamoja na makosa mengine ya uchochezi.

Mbali na viongozi hao, viongozi wengine wanaoshtakiwa kwenye kesi hiyo ya msingi ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, pamoja na Mbunge wa Kibamba John Mnyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527