Friday, November 30, 2018

BINTI ANYANYASWA KINGONO UWANJANI...ASHIKWA SHIKWA POLISI WAKITAKA ARUDI NYUMBANI

  Malunde       Friday, November 30, 2018

Muonekano wa Uwanja wa Veltins siku ya mchezo huo Novemba 24, 2018.
Binti ambaye ni shabiki wa mchezo wa soka nchini Ujerumani ameripoti polisi tukio la kunyanyaswa kingono akiwa kwenye uwanja wa Veltins wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani 'Bundesliga' kati ya wenyeji Schalke 04 dhidi ya FC N├╝rnberg.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema alikuwa amekaa na mashabiki wa kiume kwenye mchezo ambao ulifanyika Jumamosi iliyopita Novemba 24, ndipo wakaanza kumshika sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kutaka kumvua nguo za ndani.

Ameieleza polisi katika mji wa Gelsenkirchen kuwa alijaribu kuwaambia maafisa wa usalama waliokuwa uwanjani lakini hakupata msaada zaidi ya kuambiwa kuwa kama hapendi aende nyumbani akaangalie mechi kupitia runinga.

Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ambapo wameweka wazi kuwa katika malalamiko yake, binti amesema alifikia hatua ya kuvuliwa Sidiria na mashabiki hao.

Kwa upande wa klabu ya Schalke 04 nayo imeweka wazi kuwa imeanza uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini mhusika na kuchukua hatua kwa kushirikiana na polisi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post