KANGI LUGOLA AIBUKIA ZANZIBAR..AKUTANA NA RAIS SHEIN


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameibuka visiwani Zanzibar kwa ajili ya ziara ya Kikazi visiwani humo ambapo amekutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein.

Waziri huyo amekutana na Rais wa Zanzibar Dkt Shein leo novemba 19 ikulu ambapo alifika ofisini kwa kiongozi huyo wa nchi kwa nia ya kujitambulisha akiambatana na baadhi ya viongozi wake wa wizara.

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Kangi Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Kailima Ramadhani.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kangi Lugola kuwasili visiwani humo tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli kushika nafasi hiyo julai 1 mwaka huu baada kuenguliwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kudhibiti ajali za barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527