LOWASSA AZUIWA POLISI


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amezuiwa kumuona kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe anayeshikiliwa na polisi tangu jana Oktoba 31, 2018.


Msaidizi wa waziri mkuu huyo wa zamani, Aboubakary Liongo amesema kuwa leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 saa 9 Alasiri Lowassa alikwenda kumuona Zitto kutaka kujua hatima yake, kwani wako pamoja naye kuhakikisha haki inatendeka, lakini akaelezwa kuwa muda wa kumuona umeshapita.

Baada ya kufika kituoni hapo, msaidizi wa Lowassa alikwenda kuomba kibali cha kumuona Zitto lakini alielezwa kuwa muda umekwisha, ambapo Lowassa amenukuliwa akisema, “Huyu ni kiongozi mwenzetu huku upinzani lazima tushikamane kukabiliana na lolote lililo mbele yetu, tunahitaji kuwa kitu kimoja kuliko wakati mwingine wowote".

Zitto yupo kituo cha polisi Mburahati ambako alipelekwa jana baada ya kutolewa kituo cha kati Polisi makau makuu akitokea kituo cha Osterbay alikohojiwa kwa zaidi ya saa 3 baada ya kukamatwa akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam.

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post