LESOTHO YAILAZIMISHA TAIFA STARS 1 - 0


Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepoteza nafasi ya kufuzu moja kwa moja michuano ya AFCON hii leo baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji Lesotho.
Mchezo wa Lesotho na Taifa Stars
Mchezo huo uliokuwa mkali na mashambulizi mengi katika vipindi vyote viwili, uliamuliwa kwa Lesotho kuibuka na ushindi huo kupitia kwa Nkau Lerotholi katika dakika ya 76 ya mchezo na kufifisha matumaini ya Stars kufuzu michuano hiyo.
Kwa matoke hayo, sasa Lesotho inafikisha alama tano sawa na Taifa Stars yenye alama hizo huku Lesotho ikiwa nafasi ya pili ikiizidi Stars iliyopo nafasi ya tatu kwa uwiano wa mabao ya kufungwa na kufunga. Nafasi ya mwisho inashikiliwa na Cape Verde yenye alama nne.
Taifa Stars inahitaji kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uganda huku ikiiombea Cape Verde ipate ushindi dhidi ya Lesotho ili iweze kufuzu kwa tofauti ya alama moja. Matokeo tofauti na hayo, Taifa Stars itakosa nafasi ya kufuzu michuano hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post