MFANYAKAZI WA TTCL AUAWA KWA KUPIGWA JIWE SHINYANGA


Bupe Jacob enzi za uhai wake

Mfanyakazi wa Kampuni ya simu TTCL mkoa wa Shinyanga aitwae Bupe Jacob maarufu kwa jina la Mwakibibi (48) ameuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mme wake aitwaye Shyrock Kimaro (48) mwendesha bodaboda mkazi wa Ibadakuli mjini Shinyanga. 


Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ,ACP Alchelaus Mutalemwa tukio hilo limetokea Novemba 5,2018 majira ya saa 12 jioni katika Mtaa Miti Mirefu kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga. 

Amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya Shyrock na mkewe Bupe ambao walitengana hivi karibuni. 

"Siku ya tukio Bupe alimpigia simu mme wake akiomba pesa za matumizi ya mtoto lakini simu haikupokelewa,na baada ya mme kuona missed calls nyingi akamfuata mwanamke,wakaanza kujibizana na kusukumana, Bupe akaaanguka chini mme aliyekuwa amelewa akachukua jiwe na kumpiga mkewe kichwani,akafariki dunia”,amesema Kamanda Mutalemwa. 

Amesema tayari jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa na atafikishwa mahakamani. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527