MAANDALIZI YA MBEZI FUN RUN YAKAMILIKA,CHAMA CHA RIADHA NCHINI (RT) CHATOA BARAKA


Pichani kati ni mwenyekiti wa bonanza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo anaeleza kuwa kwa asilimia 90 yamekamilika,kulia ni Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau na kushoto ni mwakilishi kutoka kitengo cha afya Wilaya ya kinondoni Getruda Kafuko, kwa niaba ya mganga .
Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana kuhusu kukamilia kwa maandalizi ya mbio hizo a kwa asilimia 90 mpaka Sasa,na kuongeza kuwa vitakuwepo vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

"Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi wa ufundi wa mbio za Mbezi Fun Run Isihaka Mlawa akionesha kibali walichopewa mara baada ya kufuata na kukamilisha taratibu zote kutoka chama cha Riadhaa nchini (RT).

CHAMA cha Riadhaa nchini (RT), kimetoa baraka kwa wandaaji was mbio za kujifurahisha Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika Desemba Mosi jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai alisema RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote."Tumewataka baada ya tamasha lao, wawasiliane na RT ili mbio zao ziingizwe kwenye kalenda ya mwaka ya matukio ya RT."alisema.

Kwa upande wa waandaji hao kupitia kwa katibu Mbezi Fun Run Omary Kimbau alisema mandalizi ya mbio hizo yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka Sasa, na kwamba kuanzia leo wataweka wazi vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

"Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.

“Kama mnavyojua siku hiyo ya Desemba Mosi itakuwa ni siku ya ukimwi duniani hivyo pia tumemualika Waziri Ummy Mwalimu awe mgeni rasmi na tutafanya nae mazoezi ya pamoja, na pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu.“Damu salama inahitajika kwenye banki ya damu, kama haijanisaidia mimi itamsaidia ndugu yangu, jamaa au mtanzania yoyote yule, hivyo tumeona siku hiyo pia tuitumie kuchangia damu salama na pia kupima afya yetu kwa kupima maambukizi ya virusi ya ukimwi.”alisema.

Naye mwakilishi kutoka kitengo cha afya Angaseege Getruda Kafuko, akizungumza kwa niaba ya mganga Mkuu wilaya ya Kinondoni alisema wamefurahishwa na uamuzi wa waandaaji wa Mbezi Fun Run kuona umuhimu wa kuchangia damu."Kupima afya pia ni jambo zuri hasa kwa wanaume, kupitia Kampeni ya Afya yangu, wajitokeze kwa wingi ili wajue afya zao na kuelimishana kuishi katika mtindo bora wa maisha." alisema.

Naye mkurugenzi wa ufundi wa mbio hizo Isihaka Mlawa akizungumzia njia watakazopita wakimbiaji hao alisema mbio zitakua za kilomita 15, 10 na kilomita tano.Alisema kwa upande wa Kilomita 15 wakimbiaji wataanzia Ramada hotel, hadi clouds fm, kushukia barabara ya tank bovu, na kurejea Ramada.Wakati wa Kilomita 10 wataanzia Ramada hadi njia panda ya kwa Kusaga na mkurejea Ramada wakati wale wa Kilomita tano wataanzia Ramada mpaka Rainbow na kurejea Ramada.

Kwa upande wa mwenyekiti wa bonaza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ alisema ni wakati sasa watanzania kufanya mazoezi na ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo sukari na shinikizo la damu.“Bonaza hili linajumuisha wana Dar es Salaam yoyote atakayependa kushiriki, lengo ni kujumuika pamoja na kufahamiana, mbali na kukimbia pia kutakuwa na burudani nyingine nyingi ikiwemo mashindano ya kucheza mziki na michezo mbali mbali ya watoto.”alisema Loraa.

Alisema burudani katika bonaza hilo itatolewa na K- Mondo Sound na Up town intertaiment.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527