DIAMOND, RAYVANNY NA NANDY WASHINDA TUZO ZA AFRICAN ENTERTAINMENT AWARDS USA 2018 HUKO MAREKANI

Muimbaji wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameshinda tuzo mbili za African Entertainment Awards USA 2018 zilizofanyika October 20, New Jersey Nchini Marekani.


Msanii huyo kutokea WCB ameshinda kwenye vipengele vya Best Collaboration Of the Year kupitia wimbo wake uitwao AfricanBeauty ambao amemsjirikisha Omarion kutoka Marekani, pia ameshinda kama Best Male Artist of the Year.

Pia DJ wa Diamond Platnumz, Rommy Jones ameshinda kwenye kipengele cha Best Dj of the Year.

Msanii mwingine kutokea WCB, Rayvanny amefanikiwa Kushinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha ya Best Vocalist of the Year. Huku Nandy akishinda kama Best Single Female kupitia wimbo wake uitwao Kivuruge.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post