TAMASHA LA 'URITHI FESTIVAL' LAZINDULIWA VIWANJA VYA MAKUMBUSHO DAR | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 2, 2018

TAMASHA LA 'URITHI FESTIVAL' LAZINDULIWA VIWANJA VYA MAKUMBUSHO DAR

  Malunde       Tuesday, October 2, 2018

Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Profesa Audax Mabula ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Urithi Tanzania
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi. Devotha Mdachi akitoa neno la Shukurani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi Jijini Dar es Salaam.
Bi. Perpetua Ishika (Kushoto) akitoa maelezo mbalimbali kuhusiana na Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania na kuwasihi watanzania kuchukua fursa na kujiunga katika chuo hicho. Kulia aliye vaa suti nyeusi ni Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania.
Afisa Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania Bw. William Haule(kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na kazi mbalimbali wanazozifanya kuhusiana na maswala ya Utalii pamoja na maelezo mafupi yaliyohusu Maonesho makubwa ya Swahili International Tourism Expo (SITE!), litakalo anza tarehe 12 hadi 14 Octoba 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar.
Bi. Monica Mutoni ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(Kushoto aliyeshika Mic) akitoa maelezo mbalimbali kuhusu uhusiano baina ya hali ya hewa na Utalii, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wachoraji aliyefika katika Tamasha la Urithi Bw. Vicent Temu akitoa maelezo kuhusiana na kazi yake ya uchoraji wakati Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali.
Hii ni Moja ya picha ambayo imechorwa na Bw. Vicent Temu ambayo ametumia penseli pekee.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi. Devotha Mdachi akitazama na kupata maelezo katika moja ya picha iliyochorwa na Vicent Temu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Roots and Shoots wakitoa maelekezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na kazi mbalimbali za sanaa wanazozifanya kwa kutumia vitu mbalimbali iliwemo na ma Box, Mbao, Shanga, Ngozi na vitu mbalimbali.
Bi. Deborah Mjata ambaye ni Mbunifu kwa njia ya Kuchonga(aliyeshika Mic) akimpa maelezo Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania(aliyevaa Suti nyeusi) alipotembelea Banda hilo.
Bi. Debora Mjata Afisa Masoko wa Rike Enterprises (wa katikati) akitoa zawadi ya Sanamu aliyoichonga yeye mwenyewe kwa niamba ya Kampuni yao ya Rike Enterprises kwa Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania (kulia), na kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi Devotha Mdachi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi. Devotha Mdachi (wa pili kutoka kulia) akitazama kazi mbalimbali za wabunifu kwa kutumia Batiki.
Mgeni Rasmi Bw. Abdukadir Luta Mohamed, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wadau wa Utalii Tanzania(aliyevaa Suti nyeusi) akitazama ubunifu wa moja ya wadau wa sanaa anayefinyanga vitu mbalimbali kwa kutumia udongo na unga wa Mbao.
Hawa ni vijana wanaotengeneza vitu vyao kwa kutumia Ngozi.

Hii ni ofa maalum iliyotolewa ukiwa katika viwanja vya makumbusho Jijini Dar es Salaam ambapo Tamasha la Urithi linaendelea kufanyika utapata ofa Maalum ya kula nyama pori, na hii hapa ni nyama ya Nyumbu.


Watu mbalimbali wakiwa katika Tamasha la Urithi wakati wa Uzinduzi Jijini Dar es salaam Tar. 1.10.2018.

Picha na Fredy Njeje
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post