KOMU : SIJAWAHI KUOMBA KUJIUNGA CCM, POLEPOLE NI MUONGO


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu amemkosoa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole akidai kiongozi huyo ni muongo na hajawahi kuongea naye mipango ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Komu amesema kuwa tangu awe mbunge amekutana na Polepole mara moja tu na hajawahi kuzungumza naye kuhusu jambo lolote. 

“Polepole ni muongo sana licha tu ya kuhusiana na jambo hili, hata masuala mengine sitaki kuongea naye hata kidogo, lakini hata kama ningeomba kujiunga na CCM na wangenikatalia ni ubaguzi wa namna yake kama ingekuwa ni kweli, mtu anapojiunga na chama hakuna vigezo kama anafanya kitu gani kwenye majimbo yao.” 

Aidha, amesema kuwa yeye na Kubenea walishasema kuwa hawawezi kwenda CCM, na kama analifahamu jimbo lake vizuri asingeweza kuzungumza kitu kama hicho. 

Hata hivyo, mwishoni mwa juma lililopita akiwa katika moja ya mikutano ya CCM katika wilaya Temeke Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema wamewalazimisha waliokuwa wasema ukweli waombe samahani, wangekuwa wazuri wameomba kuja lakini wamewakatalia kwasababu kwenye majimbo yao hawatoshi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527