SERIKALI YATANGAZA MAAMUZI MAGUMU KWA MADEREVA WA MAGARI YA SERIKALI

Na.Alex Sonna,Dodoma
Kufuatia ongezeko la magari yanayoendeshwa na madereva wa Serikali kupata ajali, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limeibuka na kutoa tamko la kufuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari ya viongozi wa Serikali wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.


Akizungumzana na waandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hamadi Masauni wakati akitoa tamko la kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwa baraza hilo huku akiwa ameongoza na Makamu Mwenyekiti wa baraza,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa na wajumbe wengine wa Baraza hilo.


Mhe.Masauni amesema kuwa baraza lilopita lilifanya kazi nzuri ila baraza jipya lina malengo yake ya kupunguza ajali nchini hasa za viongozi wa Serikari kwa kuwafuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari hayo wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.


Aidha amesema kuwa kwa sasa wanaishauri Serikali kutoa waraka maalum utakaosaidia kuwadhibiti viongozi ambao wanatoa maelekezo kwa madereva wakimbize magari kwa mwendokasi na malengo ya baraza hilo ni kuimarisha utendaji wa kamati za usalama za mikoa na kuweka mikakati ya pamoja ya utendaji na usimamiaji wa majukumu ya kamati hizo.


“Kudhibiti mwendokasi na kuovateki kunakofanywa na madereva wa magari kwa kuwakamata,kuwaweka mahabusu na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao hivyo kukosa sifa ya kuondesha magari hayo,”amesema Masauni


Amesema kuwa baraza hili lina malengo mengi ya kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu ukaguzi wa alama za magari,kuongeza muda wa kutoa huduma,kwa mabasi ya abiria ya masafa marefu.


Mhe.Masauni amesema kuwa Pikipiki za kubeba abiria kuwa na tela,ushauri ambao unazingatia matumizi ya vyombo hivyo barabarani,mazingira ya barabara yanayotumika na madhara ambayo yanaweza kujitokeza.


Naibu Waziri amesema kuwa kazi kubwa ya mwendelezo wa baraza jipya ni kufanya utafiti wa vyanzo vya ajali na kuchukua hatua na kuishauri Serikali hatua mbadala za kuchukua.


Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Fortunatus Muslim,aliwashangaa wale wanaohoji utendaji kazi wa Trafiki nchini katika kupiga tochi, huku akidai kwamba wao huwa hawapangiwi wafanyaje kazi kinachotakiwa ni madereva kufuata sheria


Hivyo amesema kuwa Trafiki hatakiwi kupangiwa kazi kwani wao wanafanya kazi kubwa na kuwashangaa watu wana hoji hoji tu,nawaambia nyakua nyakua inaendelea nchini kwa wale wanaokiuka sheria za barabarani.


Aidha amesema kuwa kuhusiana na misafara ya viongozi kukimbia,misafara hiyo inataratibu zake ikiwemo kuweka askari katika kingo za barabara za kuingia barabara kuu hivyo inakuwa rahisi kuzuia watu wenye magari na pikipiki kuuvamia msafara huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post