Picha : SAVE THE CHILDREN YAENDESHA KONGAMANO LA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI MKOA WA SHINYANGA

Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la AGAPE,Rafiki SDO na Manispaa ya Shinyanga limeendesha Kongamano la Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mkoa wa Shinyanga kwa kukutana pamoja na wadau wa haki za watoto kwa ajili ya kujadili changamoto za mimba na ndoa za utotoni na mazingira salama ya mtoto shuleni.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Imarisha uwezo wa mtoto wa kike; Tokomeza ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni” -Kwa pamoja tunaweza kutokomeza ukatili dhidi ya watoto wa kike’ limefanyika leo Jumatano Oktoba 1o,2018 katika ukumbi wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU).

Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo,ambalo mgeni rasmi alikuwa Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,walimu,wazazi,mashirika,dawati la jinsia,viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa haki za watoto.

Akielezea malengo ya kongamano hilo,Mratibu wa Masuala ya Ulinzi wa Mtoto wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Alex Enock alisema,kuelekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani Oktoba 11,wameona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili changamoto zinazowakabili watoto wa kike na kuzipatia suluhu.

Alisema watoto wa kike bado wanakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ndoa na mimba za utotoni lakini pia mazingira shuleni bado siyo salama sana.

Kwa upande wake Mgeni,Charles Maugira aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao huku akiwakumbusha wazazi wajibu wa kulea watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Naye Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema ndoa na mimba za utotoni zitakwisha endapo wazazi,walimu na wanafunzi watashirikiana kutatua changamoto zinazowakabili watoto.

“Ni wajibu wa walimu kushirikiana na wazazi kulea watoto,lakini pia wazazi kuweni karibu na watoto badala ya kuwaachia mzigo walimu pekee,nanyi watoto ni wajibu wenu kusema hapana kwa mambo yanayokatisha ndoto zetu”,alisema Malima.

Nao Washiriki wa Kongamano waliwatupia lawama baadhi ya wazazi hususani wa kike ambao hushirikiana na watoto wao kike kuwapatia simu za mkononi na wengine kudiriki hata kufurahia mtoto anapopata bwana/mpenzi.

Hata hivyo wanafunzi waliomba walimu waangalie adhabu mbadala kwani adhabu kama kumrukisha kichura chura mtoto wa kike hazifai lakini pia vitengwe vyumba maalum kwa kwa watoto kujisitiri na kutoa taulo laini ‘pedi’ kwa watoto wa kike.

Mbali na kuwepo kwa michezo na burudani mbalimbali,kongamano hilo pia liliongozwa mijadala kuhusu Ndoa na mimba za utotoni na mazingira salama shuleni. 

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA KONGAMANO HILO HAPA CHINI
Mgeni rasmi Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mkoa wa Shinyanga leo katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mgeni rasmi Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Masuala ya Ulinzi wa Mtoto wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Alex Enock akielezea malengo ya Kongamano la Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Masuala ya Ulinzi wa Mtoto wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Alex Enock akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mhitimu wa darasa la Saba mwaka huu katika shule ya Msingi Mwenge,Nancy Aloyce akielezea kuhusu changamoto zinazowakabili watoto wa kike ikiwemo kutosikilizwa,kutoshirikishwa na kufanyishwa kazi nyingi huku wengine wakikatishwa masomo na kulazimishwa kuolewa.
Kushoto ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akifuatiwa na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima na Afisa Elimu Sayansi Kimu Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea wakimsikiliza Nancy Aloyce.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Kike Duniani mkoa wa Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii Salome Komba akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
Kongamano linaendelea.
Wanafunzi wakiwa ukumbini.
Mwanafunzi akielezea kuhusu mazingira ya usalama kwa wanafunzi shuleni.
Mwanafunzi akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Mmoja wa wanafunzi hao akielezea  changamoto zinazowapata watoto shuleni na kuomba walimu kuangalia adhabu mbadala kwani zingine ni kikwazo kwa watoto wa kike.
Mwalimu Aikasia Daniel kutoka shule ya Msingi Ndala A katika manispaa ya Shinyanga akichangia mada wakati wa kongamano hilo.Alisema hivi sasa wanafunzi wamebuni mbinu ya kujisahihisha wenyewe na kuwalaghai wazazi kuwa wanafanya vizuri darasani hivyo kuwaomba wazazi kuwa na tabia ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni.
Mdau wa haki za watoto,Bhoke Wambura mwenye Kampeni ya Marafiki wa Bhoke 'Friends of Bhoke' akielezea namna anavyosaidia kutoa msaada wa taulo laini kwa wasichana.
Afisa Elimu Sayansi Kimu Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Afisa Elimu Sekondari manispaa ya Shinyanga,Daudi Mkumba akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Afisa Miradi wa Shirika la YWCA, John Eddy akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Kongamano linaendelea.
Mwalimu Jane Ushiva kutoka shule ya Sekondari Masekelo akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Wadau wa haki za watoto wakiwa ukumbini.
Mzazi Joyce Mrema akichangia hoja wakati wa kongamano hilo na kuwataka vijana kuzingatia masomo yao na kuacha kusingizia kuwa kukosa pedi ama kuchapwa viboko shuleni ni changamoto kubwa shuleni.
Mwanafunzi Georgitha akichangia hoja wakati wa kongamano hilo na kuwataka walimu kuepuka kuwapa adhabu ya kuruka kichura chura watoto wa kike kwani inaweza kusababisha matatizo kama mtoto wa kike atakuwa katika hedhi.
Mwanafunzi akichangia mada wakati wa kongamano hilo
Afisa Miradi wa Shirika la Young Women Leadership,Veronica Massawe akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Wadau wa haki za watoto wakiwa ukumbini.
Afisa Upelelezi kutoka Dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga, Swahiba Msangi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mwanasheria wa Manispaa ya Shinyanga Simon Jilanga akielezea kuhusu sheria za watoto na sheria za ndoa
Mwalimu Athanas John kutoka shule ya msingi Msufini akimuulizwa swali Mwanasheria wa Manispaa ya Shinyanga Simon Jilanga
Kushoto ni Mwanasheria wa Manispaa ya Shinyanga Simon Jilanga akisikiliza swali kutoka kwa Mratibu wa Masuala ya Ulinzi wa Mtoto wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Alex Enock.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Kongamano linaendelea.
Kongamano linaendelea.
Watoto wakicheza Muziki wakati wa kongamano hilo.
Mwanafunzi akionesha michoro inayoelezea changamoto zinzowakabili watoto wa kike
Mwanafunzi akielezea kuhusu michoro inayohusu changamoto anazokutana nazo mtoto wa kike.
Vijana wakionesha mchezo wa sarakasi
Burudani ya ngoma za asili ikiendelea.
Kongamano linaendelea.
Wanafunzi wakiimba wimbo.
Walimu kutoka shule mbalimbali wakiwa ukumbini.
Afisa Miradi kutoka shirika la Thubutu Africa Initiative Paschalia Mbugani akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la YADEC,Elieza Bitegeko akielezea changamoto wanazokabiliana nazo watoto wenye ulemavu.
Wanafunzi wakionesha mchezo wa igizo kuhusu ndoa za utotoni.
Wanafunzi wakionesha mchezo wa igizo kuhusu ndoa za utotoni.
Wanafunzi wakiimba shairi.
Kongamano linaendelea.
Mzazi Elias Msafiri akichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Mzazi Gaudiozi Mwombeki akichangia hoja wakati wa Kongamano hilo.

Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Vijana waki - Dance 'kucheza muziki' na kuruka sarakasi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post