DK BASHIRU AWAONYA WANA CCM WANAOTAPIKA NYONGO NA MATUSI 'WHATSAPP' .....'TUTAWASHUGHULIKIA'

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewaonya wanachama wa chama hicho wanaohamishia mijadala ya chama kwenye mitandao ya jamii akisema watawajibishwa ili kukijenga chama hicho.

Ameyasema hayo leo Oktoba 10, 2018 wakati akichangia mjadala wa kumbukizi ya miaka 19 bila Hayati Mwalimu Julius Nyerere uliofanyika katika chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Huku akiutaja mtandao wa WhatsApp, Dk Bashiru amesema miongoni mwa mambo ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere ni dhana ya kujisahihisha huku akiwaonya wanachama wa CCM kupeleka malalamiko kwenye mitandao ya jamii.

“Sisi kama chama tumeruhusu mijadala kwenye vikao, badala ya kukaa kwenye mitandao ya WhatsApp. Atakayejadili masuala ya chama kwenye WhatsApp na akatapika nyongo na matusi, tutamshughulikia. Kwa sababu tunataka kujenga,” amesema Dk Bashiru. 

Amesema hakuna uhuru wa kudharauliana, kusema uongo, kuchocheana, kudhalilishana kwa kisingizio cha kujadiliana. “Hiyo haipo na mimi ndiyo msimamizi mkuu wa taratibu za chama, ujumbe umefika,” amesema.


Na Elias Msuya - Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post