Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI KAFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU NIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Arnold Mathias Kihaule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Uteuzi wa Dkt. Kihaule unaanza leo tarehe 03 Oktoba, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kihaule alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Oktoba, 2018

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com