Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Jumbi, Sabra Ussi Khamis amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtu anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili.
Tukio la kuuawa kwa binti huyo limetokea jana Oktoba 2, 2018 majira ya saa mbili usiku wakati Sabra alipokuwa akiuza duka nyumbani kwao na ghafla alitokea kijana huyo anayesadikiwa kuwa mgonjwa wa akili Hafidh Mkubwa Suleiman (21) na kumchoma na kitu tumboni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka amesema ni kweli tukio hilo limetokea na wanaendelea na uchunguzi kubaini taarifa zaidi.