RAIS MAGUFULI AMPA POLE KENYATTA VIFO VYA WAKENYA 50 KWENYE AJALI YA BASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli amemtumia salamu za Pole Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenya kufuatia tukio la ajali ya basi iliyotokea nchini humo, ambalo zaidi ya abiria 50 wameripotiwa kufariki dunia.


Rais Magufuli ametoa salamu hizo za rambirambi kupitia ukurasa wake wa rasmi wa twitter ambapo ameandika;


“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka.”


Mapema wiki hii Rais Magufuli alipokea Shilingi millioni 125 kutoka kwa serikali ya Kenya kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post