OSHA YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA VIJANA TANGA..YATAKA USALAMA MAHALI PA KAZI UZINGATIWE

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa
 Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga 
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao 
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao
Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akimpima urefu
mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao 
Mkaguzi wa Afya (OSHA) Dkt Linda Katabari akimpima presha
mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao leo
Kutozingatiwa kwa usalama na afya sehemu za
kazi kunaweza kuleta athari kubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kutokana na kwamba wanaweza kukumbana na majanga makubwa hali inayopelekea kuathiri shughuli zao na kila siku na kujirudisha nyuma kimaendeleo.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa. 

Alisema wanatumia maonyesho hayo ya wiki ya vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa hivyo wamedhamiria kuwaeleza fursa wanazoweza kuzitumia ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. 

“Tunaangalia Usalama na Afya kwenye maeneo yao ya kazi…tunaelewa wameajiriwa lakini kuna changamoto nyingi wanazopita kutokana na kwamba wengi hawaelewi kuhusiana na mambo ya usalama na afya na kutokujua jinsi ya kujikinga na madhara hivyo tumekuja kutoa elimu”,alisema. 

Alisema elimu wanayoitoa kwenye maonyesho hayo wanaamini wananchi wakishaijua wanaweza kujiepusha na athari za kazi hata ufanisi wa kazi utaongezeka na kuongeza kipato hatua itakayosaidia kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka. 

Alisema licha ya kutoa elimu hiyo lakini wanatumia wiki hiyo kufanya upimaji wa afya, presha uzito na urefu na kutoa ushauri ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo wanayokutwa nayo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post