Wednesday, October 31, 2018

MKUU WA MKOA ATOA SIKU TANO WANANCHI WAFUTE PICHA ZA NGONO KWENYE SIMU ZAO

  Malunde       Wednesday, October 31, 2018
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kufuta video na picha za ngono zote walizonazo kwenye simu zao, ili kujiepusha kukumbana na rungu la TCRA.


Mh. Makonda ametoa wito huo leo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, na kusema kwamba ipo siku TCRA watafanya ukaguzi kugundua nani anahusika na kuvujisha video za ngono mitandaoni, na itakuwa aibu iwapo mtu mzima au kiongozi wa serikali kukutwa nazo.


“Naomba kabla ya Jumatatu wewe Mwana Dar es salaam uliyeweka picha za ngono kwenye simu yako, naomba zifute, TCRA wana uwezo mkubwa wa kufuatilia, heri wafuatilie wakute zilikuwepo lakini zimefutwa, na vile vile unaweza ukajisahau ukaacha simu bila kuweka password mtoto akachukua simu kucheza game, akakutana na picha za ngono, ni aibu”, amesema Paul Makonda.


Leo Mh. Makonda aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mkakati wake wa kukomesha ushoga na biashara ya ngono jijini Dar es salaam ambapo ametangaza kuunda kamati ya kufuatilia vitendo hivyo, ambayo amevitaja kulipa laana taifa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post