ALIYERITHISHWA NA BABA YAKE KUUA WATU KWA MAPANGA AKAMATWA SHINYANGA..AKIRI KUUA 6


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akizungumza na waandishi  wa habari leo - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog 


Mwanaume aitwaye Fikri Charles (30) anayetuhumiwa kujihusisha na mauaji ya kukata mapanga wanawake kwa imani za kishirikina amekamatwa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akijiandaa kwenda kufanya mauaji.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa baada ya kuhojiwa na polisi amedai kazi ya kukata watu mapanga amerithishwa na baba yake mzazi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Oktoba 12,2018 Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 8,2018 majira ya saa 10 alfajiri katika kijiji cha Mwadui kata ya Ibagwe wilayani Kahama.

Kamanda Mutalemwa amesema Fikiri Charles ambaye ni mkazi wa kijiji hicho,alikamatwa akiwa nyumbani kwake akijiandaa kwenda kumkata mapanga mama mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

“Mtuhumiwa amekiri kufanya mauaji kwa wanawake sita wanaohusishwa na imani za kishirikina katika mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani kwa kulipwa pesa”,alieleza.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akizungumza na waandishi  wa habari leo 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post