UJUMBE ALIOPOST MO DEWJI MTANDAONI KABLA YA KUTEKWA


Tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ambaye ni mshindi wa zabuni ya kuwekeza kwenye klabu ya Simba kwa kiwango cha hisa asilimia 49 limetikisa kila kona.

Mfanyabiashara huyo alitekwa jana alfajiri Oktoba 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay alipokwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

Kama ilivyo kwa watu wengine, Dewji ni mpenzi wa mitandao ya kijamii, amekuwa akiitumia kuandika ujumbe mbalimbali unaochangiwa na watu wa kada mbalimbali.

Siku 10 kabla ya kutekwa, bilionea huyo kijana alitumia kurasa za mitandao yake ya kijamii kutuma ujumbe mbalimbali.

Ujumbe alioutuma kwenye Ukurasa wake wa Twitter, Oktoba 10, 2018 ulisomeka hivi kwa lugha ya Kiingereza, 

"Why aren’t schools teaching students how to do taxes and personal budgeting?

Kwa kiswahili alimaanisha; Kwa nini wanafunzi mashuleni hawafundishwi kuhusu kodi na kujiwekea bajeti?

Siku hiyohiyo aliandika ujumbe mwingine, "Your ability to handle chaos determines how you progress in life. How you manage and embrace chaos will always be one of your greatest strengths."

Akimaanisha; Uwezo wako wa kukabiliana na usumbufu, ni kipimo cha namna unavyopiga hatua kwenye maisha. Jinsi unavyodhibiti na kuondoa usumbufu ndio kutafanya uwe moja ya uimara wako mkubwa."

Ijumaa Oktoba 5, 2018 mfanyabiashara huyo aliandika,"Kila jambo unaloogopa Mungu ana mpango wake. Mungu ni mkuu kuliko hofu uliyonayo. Ana mamlaka na maisha yako ya baadaye. Kuwa na imani. #JumaahKareem."

Mbali na ujumbe huo, Septemba 26, 2018 aliandika," Hamna kitu kinaua urafiki kama mikopo!

Siku mbili baadaye aliandika ujumbe unaosomeka," The jealous one is always sick, even when his body is healthy.” akinukuu kutoka kwa Swahaba wa Mtume Muhammad (S.A.W), Imam Ali ambapo kwa Kiswahili alimaanisha," mtu mwenye wivu siku zote ni mgonjwa hata kama mwili wake una afya."

Septemba 19, 2018 aliandika," Vitu vingi katika maisha vinaweza kujaribu kukuondoa kwenye malengo yako lakini usipoteze mwelekeo. Mipango inaweza kubadilika lakini kamwe sio mwisho wa safari!

Pia siku hiyo aliandika," “Pride and arrogance are the mother of all evils” Let’s pray to the Almighty GOD to make us stay away form these bad characters."

Na Charles Abel, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527