MBUNGE LEMA ATAKIWA KUJISALIMISHA POLISI

Mbunge wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema ametakiwa kujisalimisha kituo kikuu cha Polisi mkoani humo.

Mhe. Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema ametakiwa popote alipo afike polisi kabla ya nguvu kutumika kumsaka.

“Nimepigiwa simu na Polisi kwamba natakiwa kuripoti kituo kikuu cha Polisi Arusha leo bila kukosa, sijaelezwa sababu lakini wito unaonekana kuwa wa lazima sana, lakini nafikiri kupigania haki ndio linaweza kuwa kosa langu kubwa. Msiogope,” ameandika Lema.


Hata hivyo, jana jioni Mbunge huyo aliahidi kutii wito huo huku Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi akiahidi Kutoa taarifa zaidi Leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527