LADY JAYDEE AFUNGUKA KUACHANA NA SPICE

 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na wengi hupenda kumuita dada wa bongo fleva, Lady Jaydee, kwa amefunguka juu ya tuhuma za kuachana na mpenzi wake Spice, ambaye ni msanii kutoka Nigeria Spice.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Lady Jaydee amesema kwamba hajaachana na Spice, isipokuwa wawili hao wanafanya kazi ambayo inawalazimu kuwa mbali mbali kwa muda mrefu, ikichangiwa na kuwa raia wa nchi mbili tofauti. 

Jaydee ameendelea kwa kusema kwamba licha ya Spice kuwa mbali, amechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha tamasha la #VocalsNight2018, kwa kuweza kumuunganisha na UTI ambaye alikuwa MC wa siku ile. 

“Unajua sisi ni wanamuziki, na wanamuziki ni watu wa kusafiri, na hatuishi nchi moja, kwa hiyo yeye yuko kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu, ni sawa na mume na mke, mume anaenda kazini na mke anaenda kazini kwake, haimaanishi kila siku muwe mnafuatana, leo hayuko hapa lakini ni mtu ambaye nashirikiana naye kwenye mambo mengi, kama kunisaidia kumpata UTI na kuhakikisha amefika hapa Tanzania”, amesema Lady Jaydee. 

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana baada ya kuwepo ukimya kati yao na kutoonekana pamoja kwa muda mrefu.

SOURCE:EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527