MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA KWENYE KIWANDA CHA KNAUF MKURANGA- PWANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sululu Hassan akipata taarifa ya maendeleo ya uwekezaji wa kampuni ya KNAUF nchini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Tanzania, Bw. Zachopolous Georgions.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya kiwanda hicho.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu akipokelewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega wakati alipowasili katika eneo la kiwanda Mkuranga.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu akiongea na uongozi ,wafanyakazi na wageni mbalimbali katika ziara hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios akielezea macheche kwa Makamu wa Rais juu ya kiwanda hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios mara baada ya kumaliza kutoa maelezo ya kiwanda hicho.
Baadhi ya wafanyakazi na wageni wakisubiri kumpokea, Mh.Makamu wa Rais wakati alipotembelea kiwanda cha KNAUF akiwa ziarani mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga, Abdalla Ulega akizungumza machache na Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Gypsum Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios.
Eneo la kiwanda hicho.
****
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, amefanya ziara katika kampuni ya kutoka Ujerumani ya KNAUF inayotengeneza jasi (Gypsum) na vifaa vingine vya kisasa vya ujenzi na kujionea uwekezaji inaoendelea kufanya wa kuzalisha bidhaa bora za ujenzi katika kiwanda chake kilichopo eneo la Mkuranga mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo ,Mh. Samia Suluhu Hassan,ambaye alikuwa katika ziara ya kutembelea mkoa wa Pwani,alisema serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kukabiliaana na changamoto ya umeme na kuwataka wawekezaji kutangaza bidhaa zao ili watanzania wajue kuwa bidhaa walizozoea kununua nje ya nchi sasa zinapatikana nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw.Zachopolous Georgions,alimweleza Makamu wa Rais, aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa serikali katika ziara hiyo, kuwa hadi kufikia sasa kampuni tayari imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 20/- na bado inaendelea kufanya uwekezaji, ili kuhakikisha bidhaa bora za ujenzi zinazalishwa hapa nchini ili kukidhi ongezeko la masoko yaliyopo sambamba na yaliyopo kwenye nchi jirani.

Bw. Georgions, alisema kampuni hiyo imewekeza katika biashara ya jasi kanda ya Afrika Mashariki na imechagua, Tanzania kama makao yake makuu na ilianza rasmi shughuli zake nchini miaka mitatu iliyopita na tayari imeweza kuajiri watanzania kupitia uwekezaji wake.

Mkurugenzi alisema kwa sasa kampuni inatengeneza jasi kutokana na mahitaji ya wateja wake na kwa kuanzia inatengeneza Gypsum zenye ukubwa wa milimita tisa hadi 12 ambazo ni nzuri katika kukinga nyumba dhidi ya moto na unyevu unaosababishwa na maji ya mvua.

“Tunatumia teknolojia mpya ya utengenezaji wa jasi ambayo inawezesha matumizi ya chuma mahali ambako zamani zilikuwa zinawekwa mbao. Teknolojia hiyo tayari imeanza kutumika katika kiwanda cha Mkuranga pia tunatengeneza unga maalumu wa jasi ambao unaweza kutumika kwenye ujenzi hata wa nyumba za gharama nafuu”,alisema Georgions.

Aliongeza kusema kuwa KNAF Tanzania pia ina mradi maalumu wa kufundisha vijana wa kitanzania kuhusu teknolojia mpya za ufungaji na utengenezaji wa jasi na wanapohitimu wanapatiwa vyeti vinavyotambulika dunia nzima katika sekta ya ujenzi vinavyowawezesha kufanya kazi katika nchi nyinginezo duniani

KNAUF Tanzania, ni kampuni tanzu ya KNAUF yenye makao makuu Ujerumani, ikiwa na maeneo ya uzalishaji na ofisi za mauzo 150 katika nchi zaidi ya 60 ikiwa imeajiri wafanyakazi 26,000 duniani kote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527