DK. KIGWANGALLA ATOA SADAKA NZEGA


Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameahidi kusomesha watoto 5 wanaotoka katika mazingira magumu kila mwaka  ikiwa ni kama sadaka baada ya kunusurika katika ajali na afya yake kuhimarika baada ya kupata matibabu.


Akizungumza na wananchi wa Kata ya Ndala  ikiwa ndiyo mara ya kwanza kuwasili Jimboni kwake na kuzungumza na wananchi tangu alipopata ajari Agost,4,2018 mkoani Manyara alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na Mwenyezi Mungu kumponya .
Dkt. Kigwangalla akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa Serikali ,Chama na Dini kuzungumza na wananchi alisema kuwa ameamua kumtolea Mungu sadaka ya kusomesha bure watoto watano katika chuo cha Afya cha Tabora Institute fani ya Utabibu na Afya ya Jamii na wale waliofaulu kujiunga na Sekondari wanaotoka katika mazingira magumu.

Dkt. Kigwangalla alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kulazwa hospitali nakwamba ajari iliyompata alihisi kutopona ila anamshukuru Mungu kwa rehema zake za kumponya kupitia jopo la Madactari waliompatia matibabu.

"Nimesimama hapa ni kwa Rehema za Mungu bila yeye leo hii nisingekuwa nanyi nimeamua kumrudia Mungu na kumtolea sadaka ya kusomesha watoto , nilikuwa nasomesha watoto watano chuoni sasa nimeongeza idadi na kufikia kumi,na wa mazingira magumu watakaofaulu kwenda Sekondari",alisema Kigwangalla.

Aliongeza"Nilikuwa hodari sana wakutunza namba za simu za watu kichwani lakini nilipopata ajali namba zote zilifutika kichwani niliikumbuka tuu namba ya mke wangu,kwakweli sina cha kumlipa Mungu wangu kanitendea makuu namwahidi kusomesha watoto na kuwasaidia wazee kupata bima za afya", alisema.

Dkt. Kigwangalla aliwashukuru Watanzania kwa maombi yao nakwamba kwa mujibu wa Madaktari waliomtibu wamemthibitishia kuwa sasa anaweza kuendelea na majukumu yake ya kikazi huku akikumbushia maumivu yake ya awali kuwa alipata tabu ya kupumua kwani baada ya ajali kutokana na tatizo la mapafu lakini sasa ana afya njema.

Baadhi ya Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya dini walimfanyia maombi Waziri Kigwangalla na kutoa masaha zao huku wakiwakumbusha wananchi kuliombea Taifa.

Kiongozi wa dini kutoka kanisa la Waadventista Wasabato Philemon Igezo  aliwahimiza wananchi kuendelea kuwaombea viongozi walioko madarakani kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjiri la  Kilutheri Tanzania (KKKT )Bryson Mwinuka alisema kuwa Taifa linahitaji maombi zaidi kwa viongozi wakiwamo watumishi wa Serikali kwa mustakabari wa kujenga Tanzania yenye umoja na mshikamano.

Kaimu Sheikh wa mkoa wa Tabora Ramadhan Rashid alisema kuwa mwenyezi Mungu ndiye anajua hatma ya mwanadamu hivyo kila binadamu anatakiwa kumwabudu na kumtumikia katika maisha yake.

Hotuba hiyo ya Kigwangalla iliwaacha katika majonzi adhi huku Yusuph Ally alieleza kuwa baada ya kupata taarifa ya ajali  ya Mbunge wao wengi walikuwa katika hali za kuchanganikiwa na hivyo wakamfanyia maombi.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nzega, Bwana Sekiete Selemani akizungumza katika tukio hilo kwa niaba  Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kuwa Waziri Kigwangalla kabla hajapata ajali, alimweleza mikakati ya kilimo cha zao la korosho jimboni.


Mkurugenzi huyo aliwaomba wananchi wa Nzega kuendelea kumuombea kwamadai kuwa Kigwangalla amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Wananchi wake hivyo Mungu amemsaidia kupona kwake.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527