KAMPUNI YA DAGE YAWANOA VIZURI WAHITIMU 200,BALOZI WA MAREKANI NCHINI ATOA UJUMBE Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson akifungua rasmi mahafali ya wahitimu 200 ambao walimaliza mafunzo yao katika chuo cha Dage jijini Dar es salaam.
 kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke JOHN MBWANA akitoa ufafanuzi juu ya serikali kuwapa kipaumbele wahitimu hao Kwenye mikopo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage, Geovina Kiliba akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson alipotembelea baadhi ya kazi za wahitimu hao katika chuo cha Dage

Na Khadija Seif,

KAIMU balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson amepongeza juhudi za wazazi ambao wamewaruhusu watoto wao kujiunga na kupata mafunzo ya ujasiriamali na kuhitimu. Ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuwa mustakabali wa maisha yao ni  juhudi zao binafsi na si Serikali, hivyo basi waione fursa na kuifanyia kazi kwani tayari wameshapata mafunzo ya kutosha.

Petterson ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kwamba changamoto zipo na ni sehemu ya maisha na kujiamini ndio silaha tosha katika kukabiliana na maisha ili kujijengea maendeleo kwa ajili ya maslahi yako binafsi na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam John Mbwana  amewatangazia rasmi wahitimu hao kuwa Serikali inashirikiana mao bega kwa bega na tayari wametoa vipaumbele vya mikopo ambayo itawasaidia kufungua miradi yao wenyewe.

Aidha, ameeleza wimbi kubwa linalowakuta wasichana wenye umri mdogo katika wilaya hiyo na kupelekea wingi wa vijana ambao hawana ajira nakua tegemezi kwa wazazi wao.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage, Genoveva Kiliba ambayo inashughulika na kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya ujasiriamali imetoa vyeti kwa wasichana  200 jijini Dar es salaam ambao wamehitimu katika nyanja mbalimbali.

Kiliba amepongeza ushirikiano ulionyeshwa baina ya wahitimu hao pamoja na familia zao ambazo zilikubali kuingia Kwenye mafunzo hayo na kuiona fursa ya kutimiza ndoto zao .

Na amesema wengi wa wasichana hao walishapoteza malengo na muelekeo wa maisha  kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa mashuleni,wazazi kukosa fedha za kuendelea na masomo pamoja na vifo vya walezi au wazazi.

Hivyo basi mafunzo waliyopatiwa ikiwemo elimu ya kujitambua,stadi za maisha,namna ya kufanya biashara zao itawasaidia kuendesha biashara zao kwa uweledi.

Aidha, mwalimu Makene ambae amehusika kwenye kutoa mafunzo amepongeza wasichana wote ambao wamethubutu na wameweza kunyanyuka upya na kuzikimbilia fursa hizo .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post