IGP SIRRO AMJIBU LEMA KUTEKWA KWA MO DEWJ


Jeshi la Polisi nchini limesema halina uhitaji wa kuleta wachunguzi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa msaada wa matukio ya kiuhalifu yanayotokea ndani ya nchi kwa kile walichokieleza kukwepa gharama pamoja na kuita vyombo ya uchunguzi wa nje ni sawa na kulidhalilisha jeshi la polisi.

Kauli hiyo ya Jeshi la polisi imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Jeshi hilo IGP, Simon Sirro amesema kwa sasa jeshi hilo halihitaji wataalamu kutoka nje kwa kuwa lina wataalamu wa kutosha.

“Sisi tunashirikiana na interpol vizuri sana, suala la nani aje kutusaidia sisi vyombo vya dola ndio tunaweza tukaona sababu na ikiwepo tutamshauri Amiri Jeshi Mkuu ili tusaidiwe lakini kwa hali tuliyonayo sidhani kama tuna sababu ya kusaidiwa lazima tulinde heshima ya nchi yetu,” Amesema IGP Sirro

“Mimi kubwa ninalosema watanzania liaminini jeshi lenu mimi nakutana na majeshi mengi nchini tuko vizuri sana, inapofikia unaposhindwa kuamini jeshi lako wachunguzi ni walewale na weledi uleule na huyo mtu anayekuja si atalipwa leo kwanini tuwaite wachunguzi wa nje." Ameongeza IGP Sirro

Hivi karibuni kupitia kwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Godbless Lema aliisisitiza serikali kuomba msaada wa vyombo vya uchunguzi wa nje ili kufanya uchugunzi wa tukio la kutekwa mfanyabiashara, Mohamed Dewji.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post