HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUBORESHA MAJENGO CHUO CHA ST. MARK'S KUFANYIKA KESHO JIJINI DAR


Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangisha fedha za maboresho ya majengo ya Chuo cha ST. Mark's Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Agustino Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Harambee itakayofanyika kesho tarehe 20.10.2018 chuoni hapo ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndungai. Kiasi cha Tsh Milioni 800 zinahitajika katika ukarabati wa kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha St. Mark's Dkt. Peter Kopweh akifafanua jambo kuhusiana na harambee hiyo.
***


Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo ya Chuo cha St. Mark’s kilichopo Buguruni Marapa amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia
harambee kwa ajili ya kuboresha majengo ya chuo hicho kiasi cha fedha tsh Milioni 800.

Hayo yalisemwa wakati alipokuwa na mkutano na waandishi wahabari chuoni hapo ambapo alisema  uamuzi wa kuboresha majengo hayoumetokana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Kuagiza wafanye hivyo.


“Nimewaiteni waandishi wa Habari kwa lengo la kuwataka
kutusaidia kuutangazia umma kuwa siku ya jumamosi Octoba 20, 2018 tutakuwa na harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo yetu kama tulivyo
agizwa na TCU” alisema Jaji Ramadhani.


Zaidi ya Tsh Milioni 800 zinatarajiwa kuchangishwa katika
harambee hiyo itakayofanyika chuoni hapo kuanzia saa nane mchana na mgeni rasmi anatarajia kuwa Spika wa Bunge Job Ndungai. 

Kwa ambao hawatoweza kufika katika harambee hiyo wanawezapia kuchangia katika njia zifuatazo

TIGO PESA : 0677058716
CRDB BANK: 0150237155300 (HOLLAND BRANCH)

TIB : 004600000860601 (SAMORA DAR ES SALAAM)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527