IDARA YATANGAZA AJIRA MPYA 171

Watumishi wapya 513 wa kada mbalimbali za afya wameajiriwa na Serikali ili kujaza nafasi zilizoachwa na wenzao waliochaguliwa awali na kushindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi walivyopangiwa.


Watumishi hao 513 ni kati ya watumishi 6,180 walioajiriwa na kupangiwa vituo vya kufanyia kazi ikiwa ni zahanati na vituo vya afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Nchi, Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema Oktoba 5, 2018 kuwa licha Serikali kutoa ajira hizo bado kuna kada ambazo zimekosa watu wenye sifa wa kuajiriwa na Serikali.

Amezitaja kada ambazo hazijapata watu wenye sifa wakati wa shughuli ya kuajiri ni pamoja na ile ya ofisa uuguzi msaidizi daraja la pili, ofisa muuguzi daraja la pili, daktari daraja la pili, tabibu daraja la pili, na tabibu msaidizi.

Waziri Jafo amezitaja kada nyingine zilizokosa watu wenye sifa ni pamoja na nafasi ya mteknolojia mionzi, mfamasia daraja la pili na mtoa tiba kwa vitendo.

Aidha, Serikali imetangaza ajira mpya 171 za kada mbalimbali za sekta ya afya ambapo nafasi hizo zinapaswa kuombwa kuanzia Oktoba 5 2018 hadi Oktoba 12 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post